Viongozi na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya waikosha kamati ya CCM mkoa wa Mbeya kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
Hayo yamebainiwa wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahidiwa na chama cha mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015 kwa lengo la kujua utekelezaji wa ilani ya chama katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mbeya Ndg Jacob Mwakasole amesema kuwa anawapongeza viongozi na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo.
“Niwapongezi kwa usimamizi mzuri wa majengo haya kwa uaminifu kwani majengo haya yanaakisi fedha zilizotolewa , watu mmefanya vitu vyenye uhakika sisi kama mkoa tumeridhika na hiki tulichokiona, umoja wenu unadhiilisha kuwa mpo vizuri, asanteni wote kwa kazi nzuri.” Mwakasole.
Naye katibu wa CCM mkoa wa Mbeya ndg. Solomoni Itunda amesema kuwa miradi hiyo itakapokamilika kipaumbele kiwe katika kuhudumia wananchi wanyonge.
“Miradi hii imejegwa kwa gharama kubwa kwa ajili ya wanyonge hivyo kama kuna mtu amekuja kutibiwa na hana fedha za matibabu atibiwe kwanza mengine baadaye na kwa upande wa wanafunzi sitegemei kuona mwalimu anamfukuza mwanafunzi kwa kosa la kutokulipa ada, mkamate mzazi wake mkubaliane ni kwa jinsi gani mtalipa hizo ada lakini si kwa kumsimamisha mwanafunzi masomo”. Itunda
Katika ziara ya kamati ya CCM mkoa wa Mbeya miradi iliyotembelewa ni pamoja na Hospital ya wilaya, shule ya sekondari wasichana Galijembe, na ujenzi wa soko la Tunduma Road.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.