Mkuu Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amewataka wananchi wa kata ya Iwindi kuona kuwa kutoa michango ya chakula kwa ajili ya watoto wao siyo adhabu bali ni lengo la kuboresha afya za watoto iliwawe wazuri katika masomo yao.
Chalamila ameyasema hayo kwenye mkutano wa kuongea na wananchi wa kata ya Iwindi mara baada ya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.
“tunataka tubadilishe mkoa wa Mbeya watoto hawa ni viongozi wa kesho tusipo waandalia chakula bora tutatengeneza mabomu ya badaye,naomba niwaambie leo kuwa chakula kwa mtoto sio mchango, kama serikali inatoa ada wazazi mnakazi ya kuhakikisha mnatekeleza wajibu wenu”. Chalamila.
Hata hivyo mkuu wa mkoa amewahakikishia wananchi kuwa serikali ipo makini na inaendelea kuboresha miundombinu ya afya na elimu hivyo kila mwananchi anawajibu wa kuunga mkono juhudi za serikali.
Mbali na kufanya mkutano huo, mkuu wa mkoa aliweza kukagua na kutembelea ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Songwe na Malama, kiwanda cha mifuko Mbalizi pamoja na kutembelea eneo la ujenzi wa jengo la utawala katika kata ya Iwindi katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.