Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Albert Chalamila amefurahishwa na juhudi za uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata nyama na mazao yake cha Utengule.
Chalamila amesema kuwa kunaumuhimu wa kukamilisha kiwanda hicho haraka ilikuweza kunusuru afya za wafanyakazi wa machinjio ya Mbalizi.
‘Tuharakishe haraka pale mahali ni hatari kwa afya ya wafanyakazi kwani tutapoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu hata hivyo eneo la pale ni dogo, kiwanda hiki kinafursa za kutosha vijana watapata ajira,kitaongeza uwekezaji katika eneo letu ikiwemo viwanda vya ngozi na chakula cha mifugo”.Chalamila
Naye mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E. Katemba amesema kuwa kama Halmasahuri inampango wa kukamilisha hatua za awali ilikuweza kuhamisha machinjio ya mbalizi na kupeleka utengule kwani mpaka sasa halmasahuri kwa mapato yake ya ndani imepeleka jumla ya shilingi za kitanzania milioni 168,000,000/= kwa ajili ya ukamilishaji wa awali wa kiwanda hicho.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata nyama na mazao yake naye Afisa mifugo na uvuvi wa Halmsahuri ya wilaya ya Mbeya Ndg.Titus Mbijili amesema kuwa kiwanda cha kuchakata nyama na mazao yake kikikamilika kinauwezo wa kuchinja ng`ombe 400 na mbuzi 300 kwa siku, soseji za kulisha mkoa mzima, pamoja na kutoa nyama yenye kiwango na ubora.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.