Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewahimiza wamiliki wa makampuni yanayo nunua zao la pareto katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya kulipa ushuru na kodi mbalimbali za zao hilo kwa uaminifu ili serikali iweze kutekeleza majukumu yake pamoja na kuwapatie maendeleo wananchi wake kutokana na kodi hizo na kuwawekea mazingira bora wakulima.
Mhe. Malisa ambae ndiye mgeni rasmi katika kikao hicho cha pamoja kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo jengo la utawala la halmashauri hiyo na kuwahusisha wanunuzi wa zao hilo, wakulima, maafisa ugani, na madiwani kwa lengo la kupata taarifa ya uzalishaji wa zao hilo.
Akisoma taarifa ya uzalishaji wa zao la pareto kwa mgeni rasmi, mkuu wa idara ya Kilimo na Uvuvi Bw. Gidion Mapunda amesema zao lapareto ni miongoni mwa mazao yaa biashara yanayozalisha na wakulima katika halmashauri hiyo na hasa katika maeneo ya ukanda wa juu ambao hali ya hewa yake ni baridi.
Hata hivyo Mapunda ameongeza kuwa zao la pareto limeendelea kuongeza mapato ya halmashauri mwaka hadi maka ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 zaidi ya Tsh. milion 93 zilikusanywa, mwaka 2021/2022 Tsh. milion 80 na mwaka 2022/2023 Tsh. milioni 288.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.