Chanjo ya polio awamu ya pili yafunguliwa leo rasmi na mkuu wa wilaya ya mbeya Mhe Benno Malisa ambayo itaanza tarehe 26-29 mwezi huu.
Akizungumza na wajumbe wa chanjo wa Wilaya amesema chanjo ya awamu ya kwanza ilifanyika vyema na kufikia lengo ambapo asilimia 120 ya watoto walipatiwa chanjo hiyo.
Aidha amewataka waratibu wa chanjo halmashauri zote mbili kuongeza hamasa na kutoa elimu ya kutosha kwa kuwashirikisha viongozi wa vijiji, mabalozi na wenyeviti wa mitaa kwa maana wao ndo wapo karibu zaidi na wananchi wao.
Ameongeza pia lengo la chanjo ya hii ya awamu ya pili ni kama ya mwanzo kuchanja watoto zaidi ya laki 3 “watoto zaidi ya laki tatu (3) wanatakiwa kupatiwa chanjo hii katika halmashauri zote mbili yaani mbeya vijijini na mbeya jiji” alisema malisa.
Malisa amesema kuwa awamu ya kwanza mkoa wa mbeya uliongoza na kuwa wakwanza, amewashukuru viongozi wa dini na kimila kwa ushirikiano na utaratibu mzuri wa kufikisha taarifa kwa wananchi, amewaomba kuongeza hamasa ili watoto wengi kupatiwa chanjo hiyo ili watoto wetu wawe na afya nzuri ya akili.
Mkuu wa Wilaya amesema vyombo vya ulinzi na usalama vipo na vitasimamia jukumu lote la utoaji wa chanjo ili liende vyema na kufikia lengo tarajiwa. Amewapongeza wote waloshiriki zoezi la awamu ya kwanza na kuwataka juhudi ile itumike tena awamu hii ya pili.
Wito umetolewa kwa walimu wa shule za msingi kuwaandaa watoto mapema kutokana na mtihani wa darasa la nne unaoanza tarehe 25/10/2023, watoa chnjo watakuwa na siku moja tu ya kutoa chanjo mashuleni ameyasema hayo mratibu wa chanjo bi Zuhura Mohamed.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.