SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA PARETO KUANZA 2024
Mkuu wa wilaya Mbeya Mhe Benno Moris Malisa ameyaagiza makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao la pareto kuharakisha ujenzi wa shule ya sekondari tarajiwa ya wasichana ilianza kujengwa katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini, katika kata ya Ilembo.
Mhe malisa amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule hiyo, matarajio ni kuanza kupokea wanafunzi mapema mwakani 2024. “matarajio yetu shule hii ianze kupokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali ila kwa kasi hii mnatukwamisha, ntarudi tena baada ya wiki mbili” alisema malisa
Mkuu wa wilaya aliongezea kuwa halmashauri ya wilya mbeya isimamie kwa ukaribu mradi huo, na kuwapatia kila kampuni ujenzi wa darasa,maabala na bwalo la chakula na kuhusu vyoo vya wanafunzi halmashauri inatakiwa kuchukua jukum la kuvijenga vyoo hivyo.
Mhe Malisa amemtaka mhandisi wa halmashauri kufatilia upya ugawaji huo ambao awali ulifanyika na kuipa kampuni moja ujenzi wa vyoo, ambapo kampuni hiyo imeomba kubadilishiwa na badala yake kupewa jengo jingine na kuanza ujenzi.
Kufuatia maagizo hayo kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndg. Jumanne Chaula kwa niaba ya Mkurugenzi mtengaji ameahidi kuyafanyia kazi maagizo hayo na ujenzi wa vyoo utaanza.
Makampuni ambayo yanahusika na ujenzi huo ni KATI investiment & shanatec ltd, Dakabemat ltd, tan extrac, maua py, PCT Mafinga na Pyteck ltd.
Mkuu wa wilaya aliwapa nafasi Wananchi wa kata ya ilembo waliojitokeza kwa wingi na kutoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuwaletea shule na umeme katika kata hiyo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.