Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya Mbeya ndugu Stephen E. Katemba amewataka wafanyakazi walioajiriwa hivi karibuni (ajira mpya) kutunza siri za ofisi, ameyasema hayo leo kabla ya waajiliwa hao kuapa kiapo cha maadili ya utumishi wa umma katika ukumbi mgodo wa halmashauri.
Katemba amesisitiza kuwa kwa kuchaguliwa kuwa Mtunza kumbukumbu au dereva tayari unatakiwa kujifunza kutokuongea chochote kuhusu ofisi yako kwa kufanya hivyo utakuwa umekiuka kiapo unachokula leo na kwa kukiuka kiapo adhabu kali itachukuliwa dhidi yako.
Aidha Mkurugenzi ameongeza kuwa wafanyakazi wafanye kazi kwa uadilifu ili kuzuia taharuki ambayo unaweza kuisababisha kwa kutoa taarifa za serikali kwa mtu ambaye hahusiki “fanyeni kazi kwa uadilifu kama ambavyo mmepewa mafunzo na afisa utumishi, taarifa zote za taasisi anaetakiwa kuzitoa ni mimi mkurugenzi wenu” amesema Katemba.
Mkurugenzi Mtendaji amemshukuru Dkt Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza ajira, “napenda kumshukuru Dkt Mhe Rais wa awamu ya sita (6) mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira, tangu kuingia madarakani ametoa ajira nyingi kwa sababu amona pia kunauhitaji wa rasilimali watu ili kusimamia fedha anazozitoa kwenye miradi katika halmashauri yetu kwa hiyo fanyeni kazi kwa bidii na kwa weredi” amesema katemba.
Katemba ameongeza kuwa anamshukuru sana Mhe Rais kwa kuendelea kuleta fedha katika halmashauri yetu kwa ajili ya maendeleo mbalimbali kama vile miradi ya shule za msingi na sekondari, miradi ya ujezi wa zahanati na vituo vuya afya na ukarabati wa majengo ya zamani kuyaboresha zaidi kwenye halmashauri yetu.
Waajiliwa takribani 30 wa kada mbali mbali wameletwa kwenye halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mwezi Septemba hadi Octoba wakiwemo Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa lishe, wasaidizi wa Mkurugenzi, Afisa habari, Maafisa mazingira na misitu, Maafisa kilimo na madereva.
Ndugu Katemba amewakaribisha wafanyakazi wote wapya na kutaka wafanye kazi kwa kushirikiana (team work) lakini pia upendo utawale ili kuweza kufanya vizuri kwenye kazi na kumsaidia Mhe Rais kwa ngazi walizonazo kufikia malengo ya maendeleo makubwa ya halmashauri yetu.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.