DED- SWEYA WATUMISHI SIMAMIENI MIRADI KWA WELEDI
Watumishi simamieni miradi ya maendeleo kwa weledi katika maeneo ambayo mmepatiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miaradi ya maendeleo amesema Mkurugenzi Mtendaji ndugu Paul Mamba Sweya leo Juni 25,2024 alipokuwa akiongea na watumishi wa Kata za Santlya na Iyunga mapinduzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ameanza ziara yake leo ya kuongea na watumishi wa Kata kujitambulisha na kujua changamoto wanazozipitia.
Aidha amewataka watumishi wote kujaza kazi zao kwenye mfumo wa PEPMIS maana wamebakiwa na siku nne tu kumaliza mwaka wa fedha 2023/2024. Na kuwaeleza kuwa kujaza kwao majukumu ndio kupanda kwao madaraja.
Watumishi wa Kata hizo wamefurahi kwa ujio wa Mkurugenzi katika maeneo yao, “ tunakushukuru sana Mkurugenzi kwa kuja kuonana na sisi na kutusikiliza huku ni mbali na wewe ndo mkurugenzi wa kwanza tangu nimeajiriwa mwaka 2015 sijawahi ona mkurugenzi kuja kutusikiliza Mungu akubariki sana” amesema Mtendaji wa Kata ya Santilya
Watumishi wameeleza changamoto zao kwa Mkurugenzi ikiwa ni pamoja na kuhamishwa kutoka Kata moja Kwenda nyingine bila malipo na malipo ya likizo.
Mkurugenzi Mtendaji amewaangiza maafisa Elimu Msingi na Sekondari kuweza kuwalipa watumishi hao staiki zao ndani ya wiki hii na kumuagiza afisa utumishi kusimamia malipo ya likizo za watumishi wote wa Kata hizo ambao hawajalipwa stahiki zao.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.