Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Mhe Doto Biteko, leo amewasili Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi, Ziara ambayo itahusisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya umeme Mkoani hapa.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe, Dkt Biteko amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera.
Katika kikao chake na Mkuu wa Mkoa wa MbeyaDkt. Biteko ameeleza jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katka Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Siasa na Nishati.
Katika Sekta ya Nishati, Dkt. Biteko ameeleza kuwa, upungufuwa umeme nchini ni kati ya megawati 300 hadi 190 lakini kwa sasa kuna matumaini makubwa kwani mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) unatarajiwa kuingiza megawati 235 katika gridi ya Taifa mwezi huu na matumaini mengine ni kutoka Mradi wa umeme wa Rusumo ambao utaingiza katika gridi megawati 27.
Amesema kuwa kiasi hicho cha umemekitakapoingia kwenye gridi ya taifa kitaondoa hali ya sasa ya mahitaji ya umeme kuwa makubwakuliko uzalishaji na pia kuiwezesha Serikali kuendelea kufanya maboreshokwenye miundombinu ya umeme.
Amesema kuwa kwa Mkoa wa Mbeya ambao mahitaji yake ni kati megawati 70 na 74 ambapo kwa sasa wanapata umeme wa megawati 51 na kueleza kuwa jitihada zinazoendelea sasa zitapelekea Mkoa huu pia kupata umeme kulingana na mahitaji.
Aidha Dkt Biteko amepongeaza Mkoa wa Mbeya kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi ya maendeleao, pamona na usimamizi mzuri wa sekta ya elimu ambao Watoto wanaostaili Kwenda shule wameripoti zaidi ya asilimia 70.
Dkt Biteko amesisitiza viongozikufuata agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia S. Hassan la kuwa, tofauti ya kiitikadi ya vyama vya siasa isifanye wananchi kuwa maadui bali watu wabishane kwa hoja huku kipaumbele kikiwa ni maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera amemueleza Naibu Waziri Mkuu kuwashughuli za kiuchumi katika mkoa huu zinaendelea vizuri na katika mwaka 2023/2024 mkoa ulifanikiwa kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 49 ikiwa ni zaidi ya asilimia 105.
Mhe homera ameongeza kuwa utekelezaji wa miradi ya umeme inaendelea vizuri ikiwemo ya upelekaji umeme vijijini,vitongojini na migodini. Ameongeza kuwa katika Elimu Mkoa wa Mbeya umekuwa na ufaulu mzuru huku Watoto wanaopaswa Kwenda shule , wakiripoti zaidi ya asilimia 70.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.