Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Dkt. Seleman Jafo amezitaka halmashuari nchini kujikita katika upandaji miti ili ziweze kuingiza mapato kupitia hewa ya ukaa ambayo inatajwa kuweza kuleta tija katika baadhi ya halmashauri nchini.
Akizungumza wakati wa hafla fupi kukabidhi vifaa vya mradi wa ureshwaji endelevu wa mazingira katika mabonde ya mto Rukwa na Ruaha,Waziri Jafo amesema biashara ya hewa ya ukaa ikitiliwa mkazo na halmashauri inaweza ikasaidia katika ongezeko la ukusanyaji wa mapato.
Ni hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya utekelezaji wa mradi wa urejeshwaji endelevu wa mazingira ikojolojia katika mabonde ya Ruaha na Ziwa Rukwa,hafla hiyo ilienda sambamba na shughuli ya upandaji wa miti katika hosptali ya wilaya ya Mbeya.
Waziri wa ofisi ya makamu wa Rais,Mungano na Mazingira Suleman Jafo anasema mabariko ya tabia ya nchi yamepelekea ukame na uhaba wa mvua kwa baadhi ya mikoa nchini.
Mratibu wa mradi huo Dkt Damas Mapunda anasema mradi huo unatekelezwa katika halmashauri saba za mikoa ya Mbeya,Njombe,Rukwa,Iringa na Katavi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.