Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, imeendelea kutekeleza ahadi yake ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana kila baada ya miezi mitatu. Ahadi hiyo imetekelezwa baada ya kutoa mkopo wa fedha wenye thahamani ya shilingi milioni 70.5 kwa vikundi 13 vya wanawake na vikundi viwili vya vijana.
Akikabidhi mkopo huo Kaimu Afisa Tawala Wilaya Ndg. Aron Sote kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Poul Ntinika ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo. Mbali na kuipongeza Halmashauri, pia Sote ameitaka Halmashauri kufuatilia kwa ukaribu fedha hizo kwa wanavikundi ili kuhakikisha lengo waliloliombea fedha hizo linafikiwa.
“Nimshukuru Mkurugenzi na timu yake na Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kuwajali wanawake. Lakini Mkurugenzi niombe hawa ambao leo hapa tumetoa mikopo tumewapa ni vyema tuwafualie kwa ukaribu. Maana hapa kwenye ratiba naona wote kilimo, ufugaji sijui nini ni vyema tukaenda kuona hali halisi, hivi wanavyosema viazi ni kweli je wamelima? Au wanatuweka changa la mawe hapa ili ionekane wanalima viazi kumbe wakifika nyumbani hizi hela wanagawana. Baadae inakuwa shida kuzirudisha”
Vilevile Ndg. Sote amewaambia wanavikundi wazitumie pesa hizo vizuri kwani fedha walizopewa ni mikopo na wanapaswa kuzirudisha ili ziweze kusaidia watu wengine.
“Hizi hela ni endelevu zinatoka kwenu zinaenda kwa wengine tena. Niwahase nyie mliopata hizi hela zitumieni kwenye malengo ambayo mmeombea Halimashauri, kuna mwaka Fulani niliona wameandika andiko vizuri, wamejihoredhesha majina lakini baadae tunaenda kudai zile hela inaonekana mwenyekiti na mtendaji basi. Sijui kama na hili mmeliona kama lipo naomba lizibitiwe. Wapewe walengwa kabisa na nyinyi walengwa zitumieni hizi hela kwa malengo ambayo mnayo”
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Zena Kapama amesema, Halmashauri imeweka mkakati unayoibana Halmashauri hiyo kutoa mikopo hiyo kila robo, tofauti na hapo awali ambapo ilikua inatoa kwa mkupuo. Amesema lengo la Halmashauri kuweka mkakati huo ni kuiwezesha kutekeleza kwa urahisi matakwa ya sera ya nchi inayotaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia kumi ya makusanyo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.
Mkakati huo uliwekwa na Halmashauri mwezi Oktoba, 2017. Ambapo mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 244.5 zimetolewa kwa vikundi 61 vya wanawake na vijana. Kati ya vikundi hivyo vikundi 44 ni vya wanawake na vikundi 17 ni vya vijana. Vikundi vya wanawake vimekopeshwa jumla ya shilingi milioni 181.5 na vijana vimekopeshwa jumla ya shilingi milioni 63. Fedha hizo zimekopeswa na Halmashauri kwa awamu tatu za robo ya mwaka wa fedha 2017/2018.
“Mhe. Mgeni rasmi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inamkakati wa kutoa mikopo kila robo kuanzia mwaka huu wa fedha 2017/2018 na mikopo hii inayotolewa leo inatolewa ikiwa ni ya awamu ya tatu ya mwaka huu wa fedha”. Amesema Ndg.Kapama
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.