Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imetoa mkopo wa Shilingi Milioni 174 kwa vikundi 46 vya wanawake na vijana. Kati ya vikundi hivyo vilivyopata mkopo vikundi 31 ni vya wanawake ambavyo vimepata mkopo wenye thamani ya Shilingi Milioni 121, na vikundi 15 ni vya vijana vilivyopatiwa mkopo wa Shilingi Milioni 53.
Akikabidhi mkopo huo kwa walengwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Willium Paul Ntinika ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutekeleza agizo la Serikali linalozitaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato yake kila mwaka kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanawake na vijana.
“Nitoe shukurani zangu za dhati kuipongeza Halmashauri, nimpongeze Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuendelea kutekeleza agizo la serikali, hongereni sana”
Pia Mhe. Ntinika amewataka wanavikundi waliopata mikopo hiyo kuitumia kwa tija ili lengo lililowekwa na Serikali katika kutoa mikopo hiyo liweze kufukiwa. Mhe. Ntinika amesema mikopo waliyopewa si zawadi bali wamepewa kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi na watalazimika kuirejesha baada ya kuisha siku thelathini ili wananchi wengine waliokosa mikopo hiyo awamu hii waweze kupata katika awamu zinazofuata.
“Pia naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza wanavikundi mliobahatika kupata mikopo hii kwa siku hii ya leo kwa sababu nina amini kuna wengi waliomba lakini nyie mpata bahati hii kwa hiyo bahati hii muitumieni vizuri. Nina amini mikopo hii inayokuja kwenu itafanye kazi iliyokusudiwa kwa sababu mmeandika kusudio la kuomba mkopo, mkopo huo uende sambamba na kile ambacho mlichokusidia, laniki mkumbuke kurejesha. Nilifundisha mwaka jana kwamba ukipewa mkopo pige hesabu yako kwaba kila mwezi unatakiwa kurudisha shilingi ngapi, unaziandika muda ukifika unarudisha. Hivyo basi matarajio yangu ni kwamba mikopo hii mtaanza kurejesha baada ya kuisha siku 30”
Licha ya kuwasisitiza wanavikundi kurejesha pesa walizokopa kwa wakati, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Kisemba Mwalingo amewataka wanavikundi hao kuwa wabunifu katika kufanya kazi zao ili kufikia uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kauli mbiu yakwe inayosema Tanzania ya viwanda.
“kwa bahati mbaya sana Rais anaposema Tanzania ya Viwanda watu wandani hii ni ndoto isiyotekelezeka kwa sababu hawajui ni ni maana ya kiwanda, hawajui kwamba kunaviwanda vikubwa, vya kati na vidogo. Naomba muelewe kwamba kiwanda ni kubadilisha malighafi kwenda katika kutumika. Kwamba kama ilikua pamba izae nguo, kama yalikua maembe yazae juisi. kinachofanya hivyo ni kiwanda sasa maana yangu ni nini? Maana yangu ni kwamba akinamama tunaviwanda lakini hatuvijui, kwa maana ya kuelewa neno kiwanda kila nyumba inayopika mboga na ugali ni kiwanda kwa sababu inabadilisha unga kuwa ugali”
“Kwa hiyo tunaposema kiwanda tusiwe tukafikiri ni jambo pana sana, ni jambo kubwa sana. akija mzungu hapa akapika maharage kwenye jiko, na akayaweka kwenye kopo tunasema hiki ni kiwanda lakini hakija huyu mama akipika maharage akayaweka kwenye sahani mkala hakiwi kiwanda. Kwa hiyo viwanda mnatembea navyo kazi ni kuviboresha tu, tuwe wabunifu viwe vizuri ili vipate soko.”
Awali akisoma risala kawa mgeni rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Ndg. Zena Kapama amesema kuwa, Halmashauri imeweka mkakati wa kutoa mikopo kutokana na pesa zamakusanyo ya ndani kila robo baada ya kutoa mara moja kwa mwaka kama iliyokuwa awali.
“Mhe. Mgeni rasmi katika kutekeleza azma ya Serikali ya kufikia maendeleo endelevu na malengo ya pamoja, pamoja na mkakati wa nchi yetu wa Serikali ya viwanda. Mkakati wetu Mhe. Mgeni rasmi ni kwamba kila robo tutakuwa tunatoa mikopo kwa kupitia fedha yetu ya makusanyo ya ndani kwa wanawake na vijana”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.