Menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imetenga siku mbili ya alhamisi na ijumaa kwa ajili ya kukagua ukusanyaji wa mapato.
Azimio hilo limepitishwa na kikoa cha dharura cha wakuu wa idara kilichoitishwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Oktoba 09, 2018 kilichokuwa na lengo la kubaini mikakati ya kuongeza mapato ya halmashauri.
Akipitisha azimio hilo Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Stephen E. Katemba amesema kuwa siku hizo zitatumiwa na wakuu wa idara,vitengo pamoja na watumishi wa idara ya fedha kwenda katika kata zote za halmashauri kuwatafuta watu wanaotorosha mapato pamoja na kukagua mashine za kukusanyia mapato.
“ haiwezekani kabisa, sisi tukae tu huku ofisini wakati mamilioni ya pesa yanatoroshwa huko. Sasa kila siku za Alhamisi na Ijuamaa sitaki kumuona mtu ofisini, kila mtu aende huko na aje hapa na mapato. Nawatuma mkakusanye mapato iwe kwa kulala huko au kurudi ninacho taka kuona mapato yanaongezeka"
Aidha Ndg. Katemba amewataka wakuu wa idara na vitengo kusimamia kwa umakini zoezi hilo kwa kutambua kwamba usimamizi bora wa mapato ya ndani ni nguzo muhimu kwa halmashauri katika kutekeleza nakukamilisha miradi ya maendeleo kwani mapato yakiongezeka itaisaidia halmashauri kutoka katika hali ya utegemezi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.