Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imetekeleza agizo la serikali la kutenga asilimia kumi kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi milioni 224,248,500/= kwa vikundi 14 vya wanawake na Vijana.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E Katemba amesema kuwa kwa awamu hii Halmashauri imetoa vifaa, kama mashine na pikipiki badala ya fedha taslimu ilikuwawezesha wanufaika wa mikopo hiyo kufikia malengo yao sanjali na kurejesha mikopo kwa wakati.
Akizungumza kwenye hafla hii Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Mh. Julius Ntokani ameipongeza Halmashauri kwa juhudi za kutenga asilimia kumi za mapato yake ya ndani kwa kukopesha kiasi hicho kwani ni Halmashauri chache zinazoweza kutekeleza agizo hilo.
Ntokani amewataka wale wote walionufaika na mikopo hiyo kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika namikopo hiyo.
“Mikopo hii sio zawadi ama sadaka tunawaomba Mkumbuke kurejesha mikopo hii ilikuwezesha na wengine kunufaika” Ntongani
Aidha Ntongani aliongeza kwa kusema leo tunawakabidhi mikopo hii ila naomba tusiishie hapa tunahitaji kuwatembelea mara kwa mara ilikuweza kujua na kutambua nichangamoto gani wanapitia wanapofanyia shughuli zao,
Katika hafla hiyo jumla ya vikundi 14 vime nufaika na mkopo huku 8 vikiwa vikundi vya wanawake na 6 Vikundi vya vijana.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.