Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imetekeleza agizo la serikali la kutenga asilimia kumi kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi milioni 244,613,000/= kwa vikundi 15 vya wanawake, vijana na walemavu.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E Katemba amesema kuwa kwa awamu hii Halmashauri imetoa vifaa , mashine pamoja na pikipiki badala ya fedha taslimu ilikuwawezesha wananchi kufikia malengo yao sanjali na kurejesha mikopo kwa wakati.
Akizungumza kwa Niaba ya mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Williaum Paul Ntinika ameipongeza Halmashauri kwa juhudi za kutenga asilimia kumi za mapato yake ya ndani kwa kukopesha kiasi hicho kwani ni Halmashauri chache zinazoweza kutekeleza agizo hilo.
Ntinika amewataka wale wote walionufaika na mikopo hiyo kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika namikopo hiyo.
Katika hafla hiyo jumla ya vikundi 15 vimepewa mkopo huku 8 vikiwa vikundi vya wanawake na 7 Vikundi vya vijana.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.