HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA YAPEWA HEKO
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kukusanya zaidi ya asilimia 90 ya mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Chalamila ametoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza la madiwani cha kujadili majibu ya hoja na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wahesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2016/2017 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilayaya MbeyaAgosti 17,2018.
Chalamila amesema kuwa Katika mwaka wa Fedha 2017/2018 Halmashauri ilikadiriwa kukusanya Sh. 2,867,013,000.00 na hadikufikia Juni 30, 2018 imekusanya Sh. 2,608,881,329.00 sawa na asilimia 91.00 ya lengo la mwaka na hivyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa.
“Nawapongeza sana kwa kushika nafasi ya kwanza Mwaka 2017/2018, na nawapongeza pia kwa jitihada mlizofanya mpaka kufikia asilimia kubwa ya lengo lililo wekwa kwani kwa Miaka sita (6) mfululizo makusanyo yenu ya Mapato ya ndani yamekuwa yakivuka malengo ya Makadirio au yamekuwa zaidi ya kiwango cha kilichowekwa Kitaifa cha asilimia 80. Naendelea kuwapongeza sana,”Chalamila.
Halmashauri imekuwa ikifanya vizuri katika miaka sita mfululizo kutokana na malengo na mikakati iliyojiwekea ya kuhakikiha kila mtumishi anashiriki katika zoezi la ukusanyaji wa mapato wakiwemo wakuu wa Idara.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.