Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Amelchiory Kulwizila amesema hadi kufikia Juni 1, 2018 halmashauri imekusanya jumla ya shilingi 2,304,767,856/= Ikiwa ni sawa na asilimia 81 ya mapato yake ya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 halmashauri ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi 2,867,013,000/-
Aidha, Mkurugenzi amesema kwamba, Halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha kutokana na timu aliyoiunda ya kufuatilia mapato kufanya kazi kwa umakini mkubwa kuhakikisha mapato hayatoroshwi.
Naye mwanasheria wa halmashauri, Wilson Nyamunda ambaye ni katibu wa timu ya kufuatilia mapato amesema tangu kuundwa kwa timu hiyo imeleta chachu kwa wakusanya mapato kwani imekuwa ikifanya ukaguzi wa kushtukiza jambo linalowafanya wakusanyaji kuwa makini wakati wote.
Pia ameeleza kwamba, awali kulikuwa na tatizo la kutolipwa ushuru wa huduma kwa watoa huduma hususani taasisi zilizopo ndani ya halmashauri.
“Timu ilianza kufanya ufuatiliaji kwa taasisi zote zilizopo ndani ya halmashauri. Tukabaini baadhi hazilipi ushuru wa huduma. baada ya kubaini jambo hilo tukazidai na zikalipa jambo lililosaidia kuongeza mapato ya halmashauri” Nyamunda
Aidha, Nyamunda amesema, kwa jinsi timu inavyofanya kazi kuna uwezekano mkubwa hadi kufikia Juni 30, 2018 halmashauri ikakusanya zaidi ya asilimia 95 ya mapato yake.
Aprili, 2016. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuia ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika Dodoma alitoa agizo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakusanya mapato yake ya ndani kwa asilimia 80, na zile ambazo hazitafikia lengo hilo zitafutwa kwa mujibu wa sheria.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.