“Kumbe vyanzovya ndanivikitumika vizuri vinaweza kuleta maendeleo nah ii tumeiona kupitia miradi hiituliyo tembelea iliyotekelezwa kupitia vyanzo vya mapato ya ndani” Mwalingo Kisemba mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Miradi iliyotekelezwa na inayotekelezwa kwa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya ni pamoja na ujenzi wa stendi ya Mbalizi kiasi cha shilinhi milioni 150,000,000 zimepelekwa, mradi wa ujenzi wa zahanati katika shule ya wasichana Galijembe milioni 60,000,000 zilipelekwa, Ujenzi wa ukamilishaji wa soko la tunduma road, Ujenzi wa machinjio ya muda Utengule Usongwe jumla ya shilingi milioni 25,000,000 zimepelekwa pamoja na Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja katika shule ya sekondari Usongwe kiasi cha shilingi milioni 10,000,000 zilipelekwa.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa halmashauri ilitolewa wakati wa ziara ya kamati ya fedha, uongozi na mipango yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwakwa kipindi cha robo ya tatu.
Aidha kamati hiyo ilitembelea chanzo cha maji Idimi- Haporoto unosimamiwa na RUWASA, kamati ilimshauri mwandisi wa maji kuhakikisha miti isiyo rafiki iliyopandwa kwenye chanzo hicho cha maji iondolewe kama sharia ya kuacha mita 60 toka kwenye chanzo cha maji.
Kamati imeupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya mbeya kwa kutekeleza miradi mizuri na yenyetija kwa wananchi wake na kwa kupitia mapato yake ya ndani.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.