Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana na wilaya ya Mbozi wamemaliza mgogoro wa mpaka Uliodumu kwa muda mrefu katika kitongoji cha Mtakuja hasa Uchaguzi na shughuli za kimaendeleo.
Chanzo cha mgogoro huu wa mpaka Uliibuka pale ambapo kitongoji cha Mtakuja kilipoandikishwa katika kijiji cha Mjele wilaya ya mbeya na kutangazwa katika tangazo la serikali GN la mwaka wa Uchaguzi 2014 za serikali za mitaa na Serikali Kuu badala ya kuwa kijiji cha Mtunduru kata ya Magamba wilaya ya mbozi
Afisa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya mbeya Ndg Peter Lyanga Ameeleza namna walivyo chukua hatua mbalimbali kutatua mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kufanya vikao Mbalimbali Ikiwemo cha ofisi ya mkuu wa mkoa wa mbeya,ofisi ya Mkuu wa wilaya ,Katibu tawala, Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mbeya pamoja na cha Wataalamu kutoka TAMISEMI.
Aidha Lyanga Alisema kamati baada ya kupitia,kuangalia na Kujiridhisha mipaka ya Halmashauri hizo iliamua kitongoji cha Mtakuja kilichokuwa kimeorodheswa kwa namba 451 kati ya vitongoji 931 vya mbeya kiondolewe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na kuorodheshwa katika kijiji cha Mtunduru kata ya Magamba wilya ya Mbozi.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Ndg Halipot Shega Amewapongeza Serikali za halmashauri zote mbili kwa kufanikisha kumaliza mgogoro huo wa mpaka ulio kuwa ukiwatesa kwa muda mrefu “ Sisi kama wananchi hatukatai kuwa upande wowote ule kwani wote ni watanzania.”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.