Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mh. Mwalingo Kisemba amesema kuwa kama madiwani wana imani na wataalamu katika kutekeleza shughuli na majukumu yote wakati wa kipindi chote watakachokuwa hawapo.
Mwalingo ameyasema hayo wakati wa baraza la kupokea taarifa zilizotekelezwa ndani ya halmashauri kwa kipindi chote cha uongozi wa madiwani hao kuanzia 2015 hadi 2020.
“sisi kama madiwani hatuna shaka na utekelezaji wenu wa majukumu ya kila siku kwa kipindi chote ambacho sisi hatatukuwepo, ninyi ni wachapa kazi na hayo mmetuonesha kwa kipindi hiki chote. Mmefanya mambo makubwa hivyo tunaidhinisha kuendelea kutekeleza majukumu hayo kwa niaba yetu." Mwalingo
Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya Mbeya Nd. Stephe E. Katemba amebainisha baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa kuwa ni pamoja na uidhinishaji wa upandishaji wa vyeo na ulipaji wa mishahara kwa watumishi, ujenzi wa shule ya msingi ya mchepuo wa kingeleza na madarasa kwa ajili ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanaza.
Katika kipindi cha miaka mitano halmshauri ya wilaya ya Mbeya imefanikiwa kuratibu shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospital ya wilaya, stendi ya Mbalizi, shule ya sekondari ya wasichana maalum ya Galijembe, Machinjio ya muda Utengule, vituo vya afya na zahanati pamoja na ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule za msingi na sekondari.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.