Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe . Beno Malisa akimuawakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera kwenye siku ya upandaji miti amewataka mamlaka husika kuwachukulia hatua viongozi na wote watakaojihusisha na uharibifu wa Misitu na vyanzo vya maji Mkoani Mbeya ameyasema hay oleo kwenye hafla ya uzinduzi wa upandaji miti ilofanyika kimkoa Kijiji cha Iwala kata ya Utengule Usongwe ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mhe Beno ameyaeleza haya mara baada ya zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya Sekondari Rohila iliopo katika Kijiji cha Iwala ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Akitoa agizo hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe Malisa ameendelea kuwasisitiza Wakurugenzi na Madiwani Mkoani Mbeya Kwenda kusimamia sheria zilizopo za uhifadhi wa Misitu na Mazingira ili kukomesha vitendo vya uvamizi katika maeneo hayo tengefu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ndugu Stephen E. Katemba amesema kuwa Halmashauri itaendelea kupanda miti zaidi itasaidia kutunza mazingira na kuingiza kipato kinachotokana na miti miti hiyo ambapo takribani milioni 420 imekusanywa kutokana na mazao yatokanayo na miti hii ni kwa kushirikiana na TFS.
Kwa upande wake Meneja wa TFS ksanda ya Nyanda za Juu Kusini ndugu Cosmas Ndakidemi amesema kwa mwaka huu miti itatolewa hivyo wito kwa wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujitokeza kuchukuwa miche na kupanda kwa kipindi hiki cha mvua.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.