Diwani wa kata ya Utengule Mhe. Yona Ntunjilwa akiongozana na Kaimu Afisa Elimu ndug Stanley Mwasi na ndug. Nasinyari Sablaki Mhandisi wa Halmashauri wametembelea Shule ya sekondari tarajiwa ya Ihombe katika kata ya utengule Usongwe inayojengwa kwa nguvu za wananchi.
Katika kata hiyo, Wananchi waliamua kujenga shule hii ili kupunguza adha waliyokuwanayo ya watoto wao kutembea zaidi ya kilomita 9 ili kupata elimu ya sekondari.
Shule hiyo kwa sasa imesimama kutokana na ukosefu wa fedha alisema Diwani.
Mhe. Ntunjilwa aliongeza kuwa katika mwaka wa masomo 2024 wazazi wamekataa watoto watakaochaguliwa kidato cha kwanza kutokwenda shule kutokana na umbali uliopo wa shule wanayochaguliwa.
"Wazazi wanahofu na umbali wanaotembea wanafunzi kutafuta elimu, watoto wengi wa kike hawamalizi shule hubeba mimba na wakiume wanakuwa wavuta bangi," amesema Mhe Ntunjilwa.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.