Halmashauri ya wilaya ya Mbeya inaratibu mradi wa kuwawezesha vijana waliokosa elimu ya mfumo Rasmi uitwao (IPOSA) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokosa elimu ya mfumo rasmi kuweza kujitegemea.
Mratibu wa mradi Ndg. Ismaeli Alipipi Kamendu amesema kuwa malengo ni kuwaaanda na kuwajengea uwezo wa kujitegemea vijana hao.
Kamendu amebaini kuwa mafunzo hayo yapo kwa aina mbili aina ya kwanza ni kwa wale wasio jua kusoma na kuandika na ya pili ni mafunzo ya elimu stadi ya uwezeshaji shughuli za kiuchumi kama ufundi wa magari na ushonaji wa nguo.
Akiongea na wafunzi wanao patiwa mafunzo hayo naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E. Katemba amewataka wanafunzi hao kutafusili elimu hiyo katika uhalisia wa maisha yao ya kila siku na kuwataka wale waliopata mafunzo ya kompyita kutumia elimu hiyo katika kujikwamua kiuchumi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.