Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Ndg. Zena Kapama ameitaka jamii kuienzi kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika kwani mtoto ndiye mtaalam, mtunga sera, msimamizi wa sera na kiongozi wa kesho atakaye wezesha ukuaji wa uchumi na kusimamia maendeleo ya viwanda.
Wito huu umetolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika kwa halmashauri ya wilaya ya Mbeya ambayo yamefanyika katika kata ya Lwanjilo kijiji cha Lwanjilo Juni 24, 2018.
Kapama amewashukuru wadau na mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa misaada na huduma mbalimbali kwa watoto hususani wenyeulemavu na wanaoishi katika mzingira magumu.
Wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi watoto wa shule ya msingi Lwanjilo wameikumbusha jamii kuacha tabia zote zinazokiuka haki za binadamu kama vile kutowapa elimu, kuwabagua, kuwatenga, kutowapa haki za kuishi, pamoja na kutowasikiliza .
“watoto wengi wanafanyiwa vitendo viovu kama ubakaji, ulawiti, utelekezaji pamoja na vipigo, matokeo yake watoto hawa hawaendelezwi kifikra, kiafya na kimalezi”
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika kidunia huadhimishwa tarehe 16 juni ambapo kauli mbui ya mwaka huu inasema "Kuelekea Uchumi wa Viwanda :Tusimuache Mtoto Nyuma"
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.