Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania ALAT Mkoa wa Mbeya imekagua miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mhe. DorMohamed Issa ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mbeya amesema miradi yote waliotembelea wameridhishwa nayo kufuatia hatua za utekelezaji wa miradi na kuongeza kuwa wao kama ALAT watachangia mifuko ya saruji 70 kwaajili ya kuunga mkono jitihada za kukamilisha umaliziaji wa bweni la shule ya sekondari ya Imezu iliopo katika kata ya Inyala.
Aidha Mhe. DorMohamed Issa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwakusimamia vizuri miradi iliopo katika halmashauri hiyo pamoja na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwataka viongozi wanaotoka katika halmashauri zingine kuiga mfano huo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndug. Stephen Edward Katemba ameishukuru timu ya ALAT kwakutembelea miradi hiyo na kuwapatia pongezi na ushauri mbali mbali wa kiutendaji na kwamba wao kama halmashauri wamepokea ushauri huo na kuahidi kuufanyia kazi kwa namna itakavyowekana.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.