Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imefanya ziara ya siku tatu ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo. Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni miradi ambayo imepata fedha katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018 inayoanzia tarehe 1, Julai 2017 na kuishia tarehe 30 Septamba 2017.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Mwalingo Kisemba amesema kuwa, kwa mujibu wa kanuni zinazoziongoza Halmashauri zinasema kwamba Halmashauri ni lazima iwe na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, ambayo moja ya majukumu lake ni kukagua miradi ya maendeleo.
“Halmashauri ili iweze kutekeleza majukumu yake ni lazima iwe na kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya Fedha ambayo inajumuisha wenyeviti wa kamati nyingine zote. Kamati hii inajukumu kubwa kwanza kupitisha fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Lakini pia inajukumu la kwenda “site” kukagua utekelezaji wa miradi hiyo. kazi hii inafanyika kila robo, yaani kila baada ya miezi mitatu na hii inatekelezwa kwa matakwa ya sheria”
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Julius Ntokani amesema kuwa ziara kama hiyo zinazofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango zinafaida kubwa ikiwemo kuchochea kasi ya ukamilishwaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha Mhe. Ntokani amesema kuwa faida nyingine zinazopatikana kwenye ziara hizo ni kukutana na wananchi ambapo wanapata nafasi ya kuwahasisha kuchangia juu ya ujenzi wa miradi hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri.
“Ziara hizi zinazofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, zimekuwa na faida nyingi ikiwemo kuchochea kasi ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa sababu kwenye ziara hizo tunaongozana na wataalamu wa Halmashauri, hivyo kwenye kila mradi tunapokea taarifa ya utekelezaji. Baada ya kupokea taarifa hizo tunaanza kukagu mradi. Tukisha kagua tunawaambia wataalamu mapungufu tuliyoyabaini kisha wataalamu wanayafanyia kazi hali inayopelekea miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa”
Lakini pia kwenye ziara hizi sisi kama madiwani tunapata fursa ya kukutana na wananchi, tunapokutana nao tunawaeleza faida za wao kuchangia katika miradi ya maendeleo hali inayoipelekea kuipunguzia gharama Hamashauri”
Katika ziara hiyo kamati ya fedha imeweza kukagua jumla ya miradi nane ambayo ni; machinjio ya kisasa ya Utengule, Hosteli ya wasichana Shule ya Sekondari Iwindi, kivutio cha Utalii cha chemichemi ya maji moto Ilota, daraja la Idiwili, Kituo cha Afya Isuto, jengo la Utawala Shule ya Sekondari Iyelanyala, jengo la Utawala Shule ya Sekondari tarajiwa ya Wasichana Galijembe, na shule ya Sekondari Ntonzo.
Katika iradi hiyo, miradi sita inatekelezwa na Halmashauri kwa kushirikiana huku miradi miwili ya Kivutio cha Utalii chemichemi ya maji moto Ilota na Shule ya Sekondari Ntonzo inatekelezwa na watu binafsi.
Kaimu Afisa Mipango Wilaya, Ndg. Firbert Mbwilo amesema kuwa kamati hiyo pia imepita kwenye miradi inayotekelezwa na watu binafsi kwa lengo la kujifunza. Mbwilo amesema Halmashauri inakumbana na changamoto mbalimbali wakati wa kutekeleza miradi yake, na inapaswa kutafuta mbinu za kukabilana na changamoto hizo. Hivyo Halmashauri inalazimika kutembelea sekta binafsi haswa zile zinazofanya vizuri kujifunza zaidi katika kuboresha hudama zake.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.