Kamati ya fedha,uongozi na mipango ya halmashauri wa wilaya ya Mbeya imeridhishwa na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni vituo vya afya Santilya na Ikukwa , Mradi wa maji Mbawi – jojo, Shule ya Sekondari Ileombo, Ukaguzi wa maboma katika shule mbalimbali pamoja na kutembelea Ujenzi wa hospitali ya wilaya
Kamati ilitoapongeza katika vituo vya afya Santilya na Ikukwa kwa hatua ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi licha ya kuwana changamoto ya maji pamoja na Umeme
Pia kamati imeiagiza timu ya wataalau na wasimamizi kuhakikisha wana tatua changamoto vilizopo katika vitua vya afya vya Santilya na ikukwa na kukamilisha kwa wakati ili wananchi wapate huduma stahiki na kwawakati.
Vilevile kamati ilisuluhisha kuhusu suala la kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Ilungu kwa kuwataka wazazi pamoja na wananchi kuchangia maendeleo ya taaluma kwa watoto wao, kamati iliwataka Wananchi, uongozi wa kijiji cha mashese walimu pamoja na kamati ya shule ya msingi ilungu washirikiane katika kuleta maendeleo ya shule kwa manufaa ya watoto wao.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.