Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri wa Wilaya ya Mbeya imeridhishwa na ujenzi wa vituo vya afya vinavyo jegwa kwa udhamini wa mfuko wa Serikali.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018
Baadhi ya miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na vituo vya afya vitatu vilivyopewa kiasi cha shilingi bilioni 1.7 fedha toka serikali kuu ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, vituo hivyo ni; kituo cha Ikukwa kilichopewa shilingi milioni 800, Ilembo milioni 400 na Santilya milioni 500.
Aidha kamati imeiagiza timu ya wataalamu kuhakikisha inabani kazi zilizobaki pamoja na gharama zake na kuiwasilisha halmashauri kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vituo hivyo.
Mbali na miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, miradi mingine iliyokaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na; ujenzi wa madarasa mawili katika shule msingi Italazya iliyopewa kiasi cha shilingi 3,020,000/=, ujenzi wa madarasa shule ya sekondari Ilembo iliyopewa 5,000,000/= pamoja na zahanati ya kijiji cha Usoha Muungano ambayo ilipewa kiasi cha shilingi 5,000,000/=.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.