Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya ya Mbeya leo tarehe 14 Mei 2024 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyochaguliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa ajili ya kukaguliwa,kuwekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru hapo mwezi Augusti mwaka huu.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kufika Mkoa wa Mbeya tarehe 24. 8. 2024 ukitokea Mkoa wa Tabora na kupokelewa katika Wilaya ya Chunya ambapo utazunguka kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mwenge wa Uhuru utapokelewa tarehe 30. 8.2024 katika viwanja vya shule ya Msingi Simambwe ambapo utazungukia miradi ya Elimu Sekondari, Elimu Msingi, Afya, Vyanzo vya maji na miradi ya Maji ambayo tayari maji yake yanatoka na kuwasaidia wananchi huku zikiungwa juhudi za Mhe Rais za kumtua mama ndo kichwani kwa kuwaletea maji wananchi karibu yao.
Kamati ya Ulizi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe Beno Malisa wametoa maboresho katika miradi inayohitaji kuboreshwa pia wamepongea juhudi na jitihada za Halmashauri kwenye uchaguzi wa miradi.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru hapo mwenzi wa nane, ukipokelewa Simambwe, mkesha utakuwa stendi yam abasi Mbalizi na utakabithiwa Mkoa wa Songwe katika Kijiji cha Infekenya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.