Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbeya vijijini Ndg Stephen E Katemba amemtangaza na kumpa cheti cha ushindi mgombea wa Chama cha Mapinduzi ndg. Oran Manase Njeza kuwa mshindi wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Mbeya vijijini.
Mbali na kumtangaza mshindi Katemba ametangaza matokeo ya nafasi ya ubunge katika jimbo la Mbeya vijijini kwa mchaganuo wa mgombea wa chama cha CUF ndg Edson Mwajungwa kuwa amepata kura 194 sawa na 0.2%, Chama cha NCCR ndg Jubeki Mwalugombo aliyepata kura 341 sawa na 0.4%, Philipo Mwanatega wa ACT kura 1,408 ikiwa ni 1.8%, Joseph Mjenga wa chama cha CHADEMA kwa kura 25,139 kwa 31.7% pamoja na mgombea wa chama cha mapinduzi ndg Oran Manase Njeza wa Chama Cha Mapinduzi aliye ibuka mshindi wa uchaguzi kwa nafasi ya ubunge kwa kura 52,343 kwa 65.9%.
Aidha Katika jimbo la Mbeya vijijini kulikuwa na wagombea wa nafasi 5 ya nafasi ya ubunge huku wapiga kura waliojiandisha wakiwa ni 184,495, na waliopiga kura ni 81,476 . Kura halali zilikuwa 79,425 na kura zilizoharibika zikiwa 2,051.
Na katika nafasi ya udiwani chama cha mapinduzi kimeshinda kata 27 kati ya kata 28 huku CHADEMA ikishinda kata moja na vyama vingine kutopata ushindi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.