Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ndugu Stephen E. Katemba aongoza wafanyakazi kupanda miti katika eneo la Halmashauri Iwindi, ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
“katika kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru napenda kumshukuru Mhe. Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama vile vituo vya afya, zahanati na shule za Sekondari na Msingi” alisema Katemba
Ndugu Stephen aliongeza kuwa miaka 62 ya Uhuru imekuwa ya neema kwa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa kuletewa fedha billion 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa jengo zuri na bora la utawala ambalo ndilo linatumika na wafanyakazi.
Mkurugenzi Mtendaji ameongeza kuwa kwa sasa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kila tarafa inavituo vikubwa sana vya afya. “tunamshukuru Rais Samia H. Suluhu halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kila tarafa inakituo cha afaya kikubwa, tukianzia na tarafa ya bonde la usongwe kuna kituo kikubwa kabisa cha afya cha Ikukwa chenye thamani ya shilingi milioni 800 zilizotolewa na Mhe Rais. Kituo hicho kinafanya kazi vizuri na kinasaidia watu wengi sana” alisema Katemba
Ndugu Katemba aliongeza pia halmashauri imepokea milioni 583 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari Lwanjilo ambapo kata ya Lwanjilo hakuwahi kuwa na shule ya Sekondari tangu kupata uhuru wan chi yetu.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amemshukuru Mhe Dkt Samia ambaye ni Rais na Amiri jeshi Mkuu kwa kuendeleza kudumisha amani na mshikamano ndani nan je ya nchi yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya haikuishia kupanda miti tu, sherehe hizi za uhuru zilifatiwa na bonanza la michezo ambapo asubuhi kulikuwa na mchakamchaka na baada ya hapo wafanyakazi walielekea uwanjani kwa ajili ya mchezo wa miguu, pete na mpira wa kikapu katika viwanja vya chou kikuu cha biashara (TIA).
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.