Serikali ya Jamhuri ya Muugana wa Tanzania imefuta machozi ya Maafisa Elimu kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kuwapatia pikipiki za miguu miwili.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Willium Paul Ntinika lililofanyika katika karakana ya Halmashauri septemba18,2018.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa wilaya amewataka maafisa elimu kata hao kuacha tabia ya kutumia vyombo hivyo kwa masrahi binafsi kama kubebea mkaa wafanyie shughuli zilizo kusudiwa za kuhakikisha watoto wote katikamaeneo yao wanajua kusoma,kuandika na kuhesabu.
Pikipiki zilizotolewa na kufadhiliwa na programu ya LANES yenye lengo la kufuta ujinga wa kusoma,kuandika na kuhesabu kwa watoto wa shule za msingi,ambapo pikipiki 28 zimetolewa kwa kata zote zilizoko Halmashauri ya wilaya ya mbeya zenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 84.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.