Madiwani halmashauri ya wilaya ya Mbeya wamepatiwa elimu ya namna taasisi mbalimbali za serikali zinavyo hudumia wananchi kwa kwakuwawezesha wezesha wananchi kiuchumi.
Mafunzo hayo yalifanyika katika ukimbi wa kijiji cha Inyala ambapo taasis zilizowasilisha mada za majukumu na kazi zinazo tekelezwa na taasisi hizo ni pamoja na NMB,CRDB,EQUIT BENK, NBC, POSTA BANK,TRA, VETA,TMDA,SIDO,TBS,BRELA, pamoja na kanuni za uundaji wa vikundi, mwongozo wa usajili na vigezo vya utoaji mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na walemavu iliyotolewa na afisa maendeleo ya jamii.
Akifungua mafunzo hayo makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mhe.Julius Ntokani amesema kuwa mafunzo hayo ni mhimu sana kwa madiwani kwani yatawasaidia katika kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi wanaowasimamia ikiwemo vingezo vinavyotumika katika utoaji wa mikopo.
Naye afisa maendeleo ya jamii Bi. Zena kapama amesema kuwa mafunzo haya yalilenga kuwaongezea ujunzi na uelewa madiwani juu ya mambo mbalimbali yanayo ratibiwa na taasisi za serikali kwani wao ndo mabarozi wazuri wa kufikisha ujumbe kwa wananchi kwani wananchi wengi wanapata shida ya uelewa kwa kukosa taarifa mbalimbali hususani ni zile za kanuni za uundaji wa vikundi na vigezo vya utoaji wa mikopo.
Kwa upande wa madiwani walio patiwa mafunzo hayo wamempongeza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwakufanikisha mafunzo hayo na kuomba mafunzo hayo yawezeshe tena kwa wakati mwingine kwani ni mhimu kwa jamii kujua miongozo mbalimbali ilikuweza kuwarahisishia pale wanapo hitaji huduma hizo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.