Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoani Mbeya ndug.Emmanuel Kiyabo amewataka madiwani na wataalaamu Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumiliki mali halali kadili ya uwezo wao ilikuweza kufikia Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.
Kiyabo ametoa wito huo wakati wa kutoa elimu ya kupambana na rushwa katika mkutano wa robo ya kwanza wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Oktoba 31,2018.
Pia mkuu wa taasisi hiyo amewaomba madiwani kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo pamoja na kushirikiana na taasisi hiyo katika kutoa taarifa pale ambapo patakuwa na viashiria vya rushwa.
“hakuna kosa kama la kumiliki mali ambazo hazielezeki kifungu hiki ni cha 27, lengo lake si kuwafanya watumishi wa umma kuwa masikini hapana miliki mali kadili inavyo wezekana watumishi wezangu na madiwani miliki mali lakini uweunaweza wa kuzielezea endapo utaishi maisha ya juu kuliko kipato halali utakuwa unatenda kosa tuwe na uwezo wa kuelezea mali zetu kila wakati,”Kiyabo.
Kwa upande mwingine Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mh.Julias Changani Ntokani amewaomba madiwani kutoa ushirikiano kwa watalaamu katika suala la kukusanya mapato ikiwa ni pamoja na kubaini vyanzo vipya vya mapato pamoja na kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo iliyoko kwenye maeneo yao.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.