Waheshimiwa madiwan na Mkuu wa wilaya ya Mbeya wamekabizi rimu na taulo za kike(Pedi) kwa watoto wa kike wa shule ya sekondari ya wasichana Galijembe kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Akiongea na wazazi na wanafunzi wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe.DKT. Radhid Chuachua amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanatoa mchango wa chakula cha wanafunzi.
“sitegemei kusikia mzazi analalamika kuwa hana chakula ni aibu,chakula kinacholetwa shuleni ni kile ambacho mtoto angetumia akiwa nyumbani akiwa huko usingemshindisha na njaa. kama hutaki unataka wazazi wezako wakusaidie kulea mwanao mimi kama mkuu wa wilaya sitegemei kusikia hilo.” Rashid Chuachua.
Akitoa taarifa ya shule naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg Stephen E. Katemba amesema kuwa shule imejegwa kwa nguvu za wananchi, mapato ya ndani ya Halmashauri na serikali kuu,
“shule hii imeanza mchakato wa kujegwa mwaka 2007 kwa jitiada za wananchi wazawa wa Galijembe walianza na majengo matatu lengo likiwa ni kuwa na shule maalum eneo huku likiwa limetolewa na machifu ujemzi wake ulianza rasmi mwaka 2018 kwa michango ya fedha toka serikali kuu, mapato ya ndani ya halmashauri na nguvu za wananchi mpaka sasa shule inaendeshwa kwa mfumo wa hosteli wazazi wanachangia chakula”Katemba.
Mwenyeti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mwalingo kisema amebaini lengo la kuleta vifaa hivyo kuwa ni kuboresha mazingira ya kusomea kama madiwani tuliona tujichangishe na kutoa chochote ilituweze kupata rimu na taulo za kike(PEDI) kwa ajili ya mabinti zetu.
“Mimi niliwahi kutembelea hapa nikakuta watoto wetu wanachangamoto za karatasi za kudurufia baada ya kupewa mashine ya kunakili nakala na mbunge wetu.” Mwalingo
Waheshimiwa madiwani waliwawezesha watoto hao wa kike box nne za taulo za kike na sita za rimu.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.