Mafundi watakao shindwa kumalizia ujenzi wa vituo vya Afya kwa muda uliopangwa watatolewa kwakuwa watakuwa wameshindwa kuendana na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Stephen E Katemba ametoa agizo hilo kwa timu za usimamizi wa ujenzi wa vituo vya Afya wakati alipofanya ukaguzi wa vituo vivyo vya Ilembo na Santilya vinavyo tarajiwa kukamilika kabla ya Disemba 9, 2018.
“Mafundi ambao wapo nyuma walipeni pesa yao waondoke ili wabakie kuja kwenye kutibiwa tu na mahusiano yetu na wao yabaki kwenye matibabu tu”, amesema Katemba
Aidha, Katemba ameziagiza timu za usimamizi kuhakikisha zinasimamia ipasavyo ujenzi huku akitoa siku tatu za kumalizia shughuli zilizo salia ambazo ni upakaji wa rangi kozi moja, kukamilisha mfumo wa umeme na maji.
Ametaka wajumbe wa timu hizo kuto onekana maeneo ya ofisini mpaka shughuli za ujenzi wa vituo hivyo utakapo kamilika na watendaji kuacha tabia ya kufanyakazi pale tu viongozi wanapojitokeza bali usimamizi na uchapakazi uwe endelevu.
“Nikimkuta mjumbe wa kamati hizi ofisini nitamshangaa kuwa anatafuta nini wakati ofisi yake kwa sasa ipo katika ujenzi wa vituo vya Afya na watendaji wenye tabia ya kujifanya wana chapa kazi wakituona viongozi ila tukiondoka na wao wanageuza migongo yao tutaenda nao sambamba”, amebainisha Katemba.
Ujenzi wa Vituo vya Afya vya Ilembo na Santilya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vilianza kujegwa mwezi februari mwaka huu ambavyo vimegharamiwa na mfuko wa serikali kuu pamoja na mfuko wa mapato ya ndani ya halmashauri.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.