Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ndugu Shirley Swai ameishukuru na kuipongeza serikali kwa harakati za kuazisha mpango wa elimu changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu shuleni wenye lengo la kuwakomboa vijana hao kwa kuwapatia elimu ya stadi za maisha na ujasiriamali.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa kufunga mafunzo kwa walimu watakao kuwa wanatoa elimu hiyo kwa vijana yaliyo fanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu Mbalizi.
Naye mwakilishi kutoka Taasisi ya watu wazi ndugu Placid Balige amesema kuwa elimu changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi inatolewa kwa vijana walio na umri kuanzia miaka 14 hadi 19.
Harakati za kuhakikisha tunawapa elimu vijana ambao wapo nje ya mfumo rasmi itakayo wasaidia katika kujifunza stadi za maisha, elimu ya ujasiriamali pamoja na ufundi wa awali katika fani mbalimbali ambazo zinaendana na mazingira waliyopo.
“kwa vijana ambao hawajui kusoma ,kuhesabu na kuandika naowatapata nafasi ya kuweza kufundishwa KKK kwa kuwa watapata elimu kwa kutumia mafunzo ambayo watakuwa watakuwa wanasoma stadi za KKK huku wanafanya shughuli muhimu ambazo wanaweza kufanya katika maisha” Belige.
Mwalimu Williamu Ndunguru amehitimisha kwa kusema kuwa kama walimu wataenda kuiwezesha katika jamii kwani wamesha pata elimu ya namna ya kwenda kuwafundisha na watafundisha kwa weledi kwani vijana wengi wamekosa mwelekeo wa maisha kwa sababu ya kukosa elimu na mfumo huu utaenda kuwawezesha vijana katika stadi za maisha.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.