Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ameagiza kuanzia jumatatu tarehe 25/5/2020 kuanzia saa kumi na mbili asubuhi magari yote yanapaswa kuingia mbalizi standi
Chalamila ameyasema hayo siku ya tarehe 21/5/2020 kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya, miradi aliyotembelea ni Ujenzi wa Standi ya mbalizi pamoja na Machinjio iliyopo Utengule
“Ni mwelekezea Mkurungenzi na mkuu wa wilaya kuanzia jumatatu saa kumi na mbili asubuhi magari yaanze kukatisha hapa, angalieni utaratibu wanamna magari yanaweza kupita ilivijana wetu waendelee na kazi” Chalamila mkuu wa mkoa wa Mbeya.
Pia Mkuu wa mkoa alitoa pongezi kwa watendaji wa halmashauri ya wilaya ya mbeya kwa kazi nzuri ya ujenzi wa standi ya kisasa katika mji mdogo wa mbalizi
“tuwapigie makofi watendaji wa halmashauri kwa kazi nzuri, sisi watendaji ukiangalia sio wa muda mrefu au miaka mingi lakini kwa muda tuliofika tunatekeleza yaleyaliyo ndani ya uwezo wetu”
Aidha Mkuu wa mkoa Mhe Albert Chalamila alitembelea na kukagua mradi wa machinjio Utengule ambapo ujenzi umefikia hatuo za mwisho kukamilika
“Haya machinjio naamini pamoja na kusaidia wananchi mtakuwa mmesave kosti, tujitahidi sana kuhakikisha huduma kwa wananchi wetu inakuwa ni nzuri zaidi tungee kidogo lakini utekelezaji unakuwa mkubwa zaidi” Mhe Chalamila
Pia ameutaka uongozi wa halmashauri unakamilisha kwa haraka na wakati ujenzi huo wa machinjio iliwananchi wawezekuhama pale kwenye machinjio ya zamani kwani mazingira ya pale sio mazuri sana
Wakwanza kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa Mhe Albert Chalamila na wapili ni Ndg Stephen E Katemba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na watatu ni Mhe Paul William Ntinika Mkuu wa wilaya ya Mbeya wakiwa katika ukaguzi wa Ujenzi wa Standi ya mabus Mbalizi
Masafara wa Ziara ya Mkuu wa mkoa ukipita kukagua Ujenzi wa stendi ya mbalizi wakati wa ziara ya mkuu wa Mkoa
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.