MAPUNDA- VIONGOZI ACHENE UBINAFSI KWENYE VYAMA VYENU
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ndugu Gideon Mapunda amewaasa viongozi wa Vyama vya Ushirika kutoka katika Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuacha mara moja tabia ya ubinafsi hasa ya kuangalia maslahi yao badala ya maslahi ya wakulima.
Mapunda ameyasema hay oleo Juni 25, 2024 wakati akifungua semina ya mafunzo ya kwa wanachama wa vyama vya Ushirika inayofanyika katika ukumbi wa Esta Mbalizi ambayo yatadumu kwa muda wa siku nne.
Aidha Mapunda amewaasa pia viongozi wa vyama kusitisha migogoro waliyonayo na wanachama wao kw akua kufanya hivyo kunahatarisha Uhai wa Chama na maslahi mazima.
Bi Amina Mbunde Afisa Ushirika Wilaya ya Mbeya amesema kuwa kwa vyama vyenye migogoro tayari wameshachukua taarifa zao na kuzipeleka ofisi ya Mkurugenzi na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajiri ya Utatuzi zaidi.
“tumeshapeleka taarifa kwa DED na DC ingawa kabla yah apo tulikaa nao kikao hukohuko maana kuna baadhi ya wakulima walikuwa wanadaiwa” alisema bi Amina.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.