Walimu Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wametakiwa kuacha tabia ya kuwaadhibu wanafunzi kwa kuwachapa viboko.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E.katemba wakati wakikao cha kujitambulisha kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa septemba 3, 2018.
Katemba amesema adhabu ya viboko shuleni haifudishi mwanafunzi bali inamtia uoga na kumuondolea ujasili wa kujifunza awapo shuleni. Hivyo amewakanya walimu kuacha tabia ya kuwachapa wanafunzi pindi wanapokosea na badala yake wawape adhabu zitakazowafunza zaidi kama inavyoelekezwa kwenye sheria, taratibu, kanuni, miungozo na misingi ya ualimu.
“Vibokoni marufuku katika shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,walimu wenye hulka ya kupiga wanafunzi muache tabia hiyo mara moja” Katemba.
Maagizo mengine aliyoyatoa mkurugenzi huyo katika kikao hicho ni pamoja na watumishi kuhakikisha wanafanya kazi kwabidii na kuonesha vipaji vyao katika utendaji kazi na pia amewaagiza wakuu wa idara navitengo kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa watumishi waliochini yao ilikupunguza manung’uniko maeneo ya kazi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.