Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla amesema mazingira na viwanda vinategemeana katika ustawi wake. Makalla ametoa kauli hilo Juni 5, 2018 katika kilele cha maazimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yamefanyika kijiji cha Bulyaga kata ya Bulyaga wilaya ya Rungwe.
Akitoa agizo hilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Julius Chalya amesema kwamba nchi ya viwanda itaweza kufikiwa pale tutakapoweza kutunza mazingira, kwani ustawi wa viwanda unategemea mazingira bora ili kujihakikisha usalama wa kupata malighafi.
“Ukihifadhi mazingira viwanda vinakuwa endelevu kwani viwanda hivyo vinategemea malighafi zinazopatikana kwenye mazingira hayo”
Aidha, Makalla amesema viwanda na mazingira vina uhusiano mkubwa na kila kimoja kikitumiwa vibaya kinaweza kumuathiri mwenzake. Hivyo ametoa rai kwa wananchi wote kutunza na kulinda mazingira ili kufaidi matunda ya viwanda, na wawekezaji wa viwanda kufanya uchunguzi wa athari za kimazingira kabla ya kuanzisha viwanda vyao.
Kilele cha maazimisho ya siku ya mazingira duniani uazimishwa kila mwaka ifikapo Juni 5. Kwa mwaka huu kidunia siku hii imeazimishwa nchini India ambapo kauli mbiu ya kidunia inayosema “Pinga uchafuzi wa mazingira unaotokana na bidhaa za plastiki” Kitaifa maazimisho yamefanyika jijini Dar es salaam kwa kauli mbiu inayosema “Mkaa ni gharama; Tumia nishati mbadala”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.