Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abert Chalamila amezitaka Halmashauri zote katika mkoa wa Mbeya kuhakikisha zinaongeza juhudi katikakukusanya mapato ili kufikioa malengo waliyokusudia.
Chalamila ametoa maagizo hayo katika kikao chake cha kujitambulsha kwa watumishi wa umma kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa chenye lengo la kutoa muelekeo wa kuimarisha mapato katika mkoa wa Mbeya.
Katika kikao hicho chalamila amewataka watumisha wa umma ngazi zote kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa kina wa suala la kukusanya mapato kwa kubaini vyanzo vipya.
Pia ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zina hakiki mara kwa mara mashine za kukusanyia mapato “POS” ili kuweza kuzuia mianya ya upotevu wa mapato.
Aidha amewataka watumisha wa umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kutumia vizuri rasilimali na kupinga matumizi yasiyo ya lazima .
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.