Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Martha Mgata amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika michezo kwani michezo ni taaluma na ajira.
Hayo yamebainishwa wakati wa zoezi la kupokea vikombe vinne vya ushindi wa UMISSETA kwa ngazi ya mkoa kutoka sekretarieti ya wilaya ya Mbeya lililofanyika katika ofisi ya mkurugenzi Mei 28,2018.
Akikabidhi vikombe hivyo Afisa Utamaduni na Michezo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Joseph Singundali amesema Halmashauri imepata ushindi wa kwanza katika michezo ya; mpira wa kikapu wavulana, mpira wa miguu wavulana na sanaa za maonesho. Pia Halmashauri imepata kikombe cha mshindi wa tatu katika mchezo wa mpira wa wavu wasichana.
Mashindano hayo yamefanyika kwa muda wa siku nne(4) kuazia Mei 25,2018 na kumalizika Mei 28, 2018 katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Iyunga. Jumla ya wanafunzi 120 toka shule 48 za sekondari halmashauri ya wilaya ya Mbeya walishiriki, kati yao wanafunzi 21 wamechaguliwa kujiunga na timu ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya UMISSETA kitaifa mkoani Mwanza yatakayoanza Juni 4, 2018.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.