Shule ya sekondari Iyawaya iliopo katika kata ya Inyala katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipokea kiasi cha shilingi milioni 160 za UVIKOkutoka serikali kuu kwa ajili ya kujenga vyumba nane vya madarasa ambapo vyumba hivyo vimejengwa na kukamlika na kuanza kutumika kama ilivyotarajiwa na kwa sasa shule ina kidato cha kwanza na cha pili ambapo jumla ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ni mia mbili kumi na tano (215).
Baada ya kuanza kwa shule hiyo serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ilitoa tena kiasi cha shilingi milioni 114 kwa ajili ya kujenga nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuchukua walimu wawili yaani (2 IN 1) ambapo katika ujenzi huo zilitumika kiasi cha shiliungi million 88 na kubakiwa na kiasi cha shilingi milioni 26, wananchi na uongozi wa serikali katika kata hiyo waliomba kubadilisha matumizi kiasi cha pesa kilichobaki katika ujenzi wa nyumba ya walimu zitumike kuongeza madarasa mawili 2 pamoja na ofisi ya Mkuu wa shule na wakafanya hivy na ujenzi unaendelea.
Aidha serikali kuu imetoa tena kiasi cha shilingi milioni thelathini (30) kwa ajili ya ujenzi wa maabara ambapo kwa sasa umefikia hatua ya ukamilishaji wa kufunga meza pamoja na dali, hata hivyo katika shule hiyo kuna mradi wa ujenzi wa madarasa mawili (2) unaoendelea kwa nguvu za wanachi, hivyo baada ya kukamilika madarasa hayo kutakuwa na jumla na vyumba vya ya madarasa kumi na mbili (12) katika shule hiyo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.