Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imekusudia kutumia kiasi cha shilingi million 253 kutoka mapato yake ya ndani kwa ajili kumalizia ujenzi wa vituo vya afya vya Ilembo,Santilya na Ikukwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma karibu na makazi yao.
Akizungumza na watendaji wa kata na vijiji Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ndug. Stephen E. katemba amesema vituo hivyo vilishaanza kujengwa katika mpango wa kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto hivyo kama Hamashauri hainabudu kuendelea na shughuli za ujenzi kwa kutumia mapato yake ya ndani.
Aidha katika hatua nyingine Katemba amewataka wahudumu wa afya kuhakikisha wanahudumia makundi maalumu kwa ukarimu wakiwemo wazee na watoto.
Katemba amewataka watalaamu katika Sekta ya afya na ujenzi kuhakikisha wanasimamia vituo hivyo kwa umakini na ukaribu huku akiwataka kupiga kambi ili kuweza kusimamia na kutoa ufafanuzi wa kitalaamu kwa mafundi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.