Asisitiza Halmashauri nyingine kujifunza kutoka Mbeya DC
Imeelezwa kuwa, miradi mbalimbali ya ujenzi imetekelezwa rasmi na Halmashauri ya Wilaya Mbeya DC ambapo wanafunzi wa Sekondari na Shule ya msingi watapata mazingira rafiki ya kupata elimu katika wilaya hiyo.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Deo Ndejembi mara baada ya kutembelea na kukagua maeneo ya ujenzi wa shule hizo leo Septemba 29, 2023.
“Hakika mmefanya kazi kubwa kukamilisha ujenzi wa miradi hii, Maendeleo haya ni makubwa katika kuwezesha wanafunzi wanapata mazingira bora ya elimu yao ya Msingi na Sekondari,” amesema Ndejembi.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuhakikisha watanzania wanapata fursa mbalimbali ikiwemo mazingira wezeshi katika elimu hapa nchini.
“Mhe. Rais ameleta fedha ya ujenzi hapa na sehemu mbalimbali ya nchi, fedha hizi tuzitumie vizuri katika maendeleo yetu na tumpe pongezi Rais Samia kwa kutuletea fedha katika wilaya yetu kwa ajili ya maendeleo,” amesisitiza Waziri Ndejembi.
Katika hatua nyingine, Waziri Ndejembi amesisitiza Halmashauri nyingine zijifunze kwa kufanya vizuri kama ilivyo halmashauri hii. Amesema Halmashauri hii imefanya vizuri na ni funzo kwa wengine wajifunze.
Amempongeza Murugenzi Mtendaji ndg Stephen E Katemba kwa usimamizi na ufatiliaji mzuri wa miradi hii mikubwa ambayo imegarimu 583,180,028 million.
Ziara hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya wilaya na mkoa huo pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.