Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kuandaa utaratibu utakaowashirikisha wananchi katika kuilinda na kuitunza amani kwenye maeneo yao. Makalla ametoa agizo hilo jana wakati akiongea na watendaji kata na wakuu wa tarafa wa halmashaurii ya wilaya ya Mbeya pamoja na wa jiji la Mbeya katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo jijini Mbeya.
Makalla amesema uhalifu unatendeka mitaani na wahalifu nao wanaishi mitaani, hivyo amewataka watendaji kata kuwaagiza watendaji wa mitaa na wenyeviti wa serikali za mitaa kuitisha mikutano ya hadhara ikiwa na agenda ya kujadili usalama katika maeneo yao.
“Amani ndio msingi wa shughuli zote za maendeleo, palipo na amani, maendeleo hayakosekani. Lakini amani hii tukiwaachia polisi peke yao na kuwatenga wananchi kamwe hatutafanikiwa, waelimisheni wananchi wasisite kutoa taarifa polisi, taarifa zao zitasaidia kudhibiti uhalifu usitokee” amesema Makalla.
Naye Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Mhe. Paul Ntinika akiongea katika kikao hicho amesema kwamba atahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kwa watendaji kata na wakuu wa tarafa yanatekelezwa.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.