Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewataka waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutumia madaraka waliyopewa kisheria kwa kuwasimamia ipasavyo wataalamu wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Mhe. Makalla ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano Maalum wa Halmashauri kwa ajili ya kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Wakati akitoa kauli hiyo Mhe. Makalla amesema katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipata hati yenye mashaka. Alisema tafsili ya kupata hati yenye mashaka kwa wananchi ni kamba katika Halmashauri kuna wizi jambo linalosababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao. Sasa ili kuondokana na jambo hilo ni vyema waheshimiwa madiwani waongeza nguvu katika kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
Pia Mhe. Makalla amewataka wataalamu kuongeza ufanisi katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kufuata Sheria na Taratibu za matumizi ya fedha za Umma.
“Ni lazima wataalamu wawe makini kwa kufuata sheria wakati wa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, hatutaki wataalamu wanaozalisha hoja bali tunataka wataalamu wanaoepuka hoja kwa kufuata Sheria na Kanuni za matumizi ya fedha za Umma” Amesema.
Mhe. Makalla pia amesisitizia suala la umoja kati ya Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kama suala muhimu la kufikia tija ya kuwaletea maendeleo wananchi. Amesema wananchi hawataki kuona malumbano bali wanataka kuona Halmashauri yao inapiga hatua katika maendeleo. Amesema kama kunasuala lolote limetokea ni vyema kuomba ushauri kwa viongozi wa Serikali waliopo kuanzia Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mhe. Mkuu wa Mkoa.
“Naishauri Halmashauri yenu kuwa na umoja kati yenu na watendaji, kati yenu wenyewe waheshimiwa madiwani na uongozi wa serikali, yupo Mkuu wa Wilaya yupo Mkuu wa Mkoa. Kwa hali iliyopo sasa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya msipo chukua hatua bado kuna mapungufu mengi kazi yangu kwawaambia na mimi napenda kuwaambia ukweli …kwa sababu mimi ndio msimamizi wa kwanza na kiongozi wa shughuli zote katika mkoa huu na mlezi na msimamizi wa serikali za mitaa ndio maana nipo hapa.”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.