Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika amekabidhi vitanda 31 venye uwezo wa kuchukua wanafunzi 62 kwa shule ya Sekondari Ilembo kwa ajili ya mabweni ya wasichana. Shule ya Sekondari Ilmbo iletegemewa kuanza kidato cha tano kwa mwaka 2016 lakini lengo hilo lilishindwa kufikiwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya miundombinu ikiwemo mabweni pamoja na ukosefu wa vitanda.
Akikabidhi vitanda hivyo 31 venye thamani ya Tsh Mil 5,593,751.80/= Mhe. Ntinika amesema Shule ya Sekondari Ilembo inamahitaji ya vitanda 92 kwa ajili ya kuchukua wananfunzi wa kidato cha tano, lakini vilivyopo ni vitanda 71 na hivyo kufanya upungufu kuwa vitanda 21. Amesema kati ya Vitanda hivyo 71 vilivyopo sasa vitanda 40 vimetegenezwa kwa nguvu za wananchi na vitanda 31 alivyovikabidhi kwa Mkuu wa Shule vimetolewa na Taasisi ya Kimarekani isiyo ya Kiserikali ya Mery Ryan Foundation inayofanya kazi ya kusaidia watoto yatima katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mhe. Ntinika ameipongeza Taasisi ya Mery Ryan Foundation kuwa imetekeleza kwa vitendo kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU, kwa kuchangia maendeleo ya kijamii. Amesema huo ni mfano wa kuigwa, hivyo wananchi wa kata ya Ilembo waongeza kasi ya kuchangia maendeleo ili vitanda viweze kupatina na kidato cha tano kifunguliwe katika shule hiyo ifikapo Juni 2018.
“Ndugu zetu ambao wametoa msaada huu, imekua chachu kwa wananchi wa Ilembo kuwa tayari nao kuchangia. Tunaposema HAPA NI KAZI TU wenzetu wametimiza azma ya Mhe. Rais wetu wa Tanzania Mhe. Dokta John Pombe Magufuli kwamba sisi awamu hii ya tano HAPA NI KAZI TU. Sasa tunatoa wito kwa wananchi wa Ilembo kwamba kwa muda huu uliobaki waendelee kuongeza kasi ya kuhakikisha kwamba vile vitanda ambavyo bado havijatengenezwa vinakamilika”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeye, Ndg. Amelchiory Kulwizila amesema Halmashauri yake itaendelea kushirikiana na wananchi kukamilisha miundombinu mbalimbali inayohitajika katika shule hiyo ili kidato cha tano kianze kama walivyofanya kwenye ujenzi wa mabweni ambao unaendelea kukamilishwa.
“Kwa upungufu uliopo wa vitanda 21 hiyo kwangu mimi ni changamoto ambayo nitakabiliana nayo. Nitatakiwa mimi nimalizie hivyo vitanda. Ila kwa kufuatana na hali kwa sababu Halmashauri kama unavyoona imeshaingia pale kwa kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa yale mabweni ya watoto. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana kuhakikisha kwamba mwakani lazima watoto wasome”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.