Mradi wa maji wa Izumbwe, Iwindi, Mwashiwawala unatarajiwa kukamilika mwezi juni, 2018. Kukamilika kwa mradi huu wananchi zaidi ya elfu 14 wa vijiji vya izumbwe, Iwindi na Mwashiwawala watanufaika kwa kupata maji safi na salama.
Mhandisi wa Maji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Vivian Mndolwa amesema mradi huu ulianza kujengwa mwezi Machi, 2017 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Disemba 2017. Lakini kutokona na mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha mradi kusimama kwa muda hivyo utamalizika mwezi Juni, 2018.
“Mradi huu ulianza kutekelezwa machi 2017 na mkataba wa mradi huu ni wa miezi 9. Na tulitegemea tungemaliza mwezi wa 12 lakini kwa sasa tutamaliza mwezi Juni 2018… kwa sababu mamboa yote yapo, isipokuwa kilichokuwa kinazuia ni hizi mvua zinazonyesha wangechimbwa mitalo ingekuwa inajifukia”
Gharama za mradi huu ni Shilingi bilioni 1.5 ambapo mpaka sasa pesa zilizotumika ni Shilingi Milioni 562,122,764/- Kazi zilizofanyika ni ujenzi wa matanki yote matatu yenye ukubwa wa lita 45,000, 90,000 na135,000. Ujenzi wa vituo 38 vya kuchotea na ununuaji wa mabomba ya usambazaji maji yenye urefu wa mita 61,213. Kazi zilizobaki ambazo hadi kufikia Juni, 2018 zitakuwa zimekamilika ni ujenzi wa vituo vingine 38 vya kuchotea maji pamoja na ulazaji wa mabomba.
Diwani wa Kata ya Igale, Mhe. Maiko Mwasonzwe ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutekeleza mradi huu ambao ni muhimu kwa wananchi wakata yake pamoja na kata jirani ya iwindi. Mhe. Mwasonzwe amesema mradi huu utakakapo kamilika utakuwa ni suluhisho la kudumu la tatizo la maji katika eneo lake kwani wananchi wamekuwa wakipata hadha kubwa ya ukosefu wa maji.
“Wananchi wameusubiri mradi huu kwa muda mrefu na wanapata shida ya kutafuta maji naamini kwamba mradi ukikamilika itakuwa ni mkombozi kwa wanachi wangu wa kata ya igale na kata ya Iwindi ambao wanategemea mradi huu wa maji”
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Izumbwe ambao nao ni wanufaika wa mradi huu pindi utakapokamilika wamesema kuwa tatizo la maji tatizo la maji katika kijiji chao linaenda kuwa historia. Hivyo wamesemapindi mradi huo utakapo kamilika kufika mwezi Juni wataupokea kwa furaha, lakini kubwa zaidi watautunza mradi huo kama wanavyotunza miradi mingine inayotekelezwa na Serikali katika kijiji chao. Dick Paulenje mkazi wa kijiji hicho amesema
“Huu mradi ukikamilika kufikia mwezi wa sita tutaupokea vizuri sana kuufurahia kwa sababu tutakuwa tunanufaika na uhitaji wa maji yenyewe maana maji yanauhitaji mwingi tu, kuna kumwagilia, kupikia na mengine mengi tu ya kibinadamu, nadhani yatakuwa yametusaidia sana na niahidi sisi kama wananchi tutautunza mradi huu illi kulifanya tatizo la maji kuwa historia katika kijiji chetu”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.